Maswali & Majibu

Nyansaho Foundation inatizamia zaidi kusaidia nini katika jamii?

Tuna dhamira madhubuti ya kusaidia katika nyanja tatu tofauti ambazo ni elimu, afya, na utokomezaji wa umasikini.

Je, taasisi au kampuni zinaweza kushirikiana na Nyansaho Foundation?

Ndiyo! Tunakaribisha ushirikiano kutoka kwa kampuni, mashirika na taasisi mbalimbali. Jaza fomu ya ushirikiano wa kibiashara na tutawasiliana nawe.

Mchango wangu unatumiwa vipi na shirika?

Mchango wako unatumiwa moja kwa moja katika miradi kama kugawa vifaa vya shule, huduma za afya, maji safi, na maendeleo ya jamii. Tunazingatia uwazi na uwajibikaji.

Nyansaho Foundation inafanya kazi maeneo gani?

Tunafanya kazi katika maeneo ya vijijini na yasiyo na huduma bora nchini Tanzania, tukijikita kwenye elimu, afya, na kupunguza umasikini.

Ninawezaje kujitolea kufanya kazi na Nyansaho Foundation?

Unaweza kujisajili kwa kujitolea kupitia fomu ya kujitolea kwenye tovuti yetu. Baada ya kujisajili, timu yetu itawasiliana nawe kuhusu nafasi zilizopo.

Je, hukupata majibu ya swali lako? Tuulize hapa moja kwa moja!

info@nyansahofoundation.or.tz
+255 7** *** ***
Dar es salaam, Tanzania
Fungua ramani
Inatuma
Swali lako limetumwa. Asante sana!